|
Hapo zamani za kale kulikuwa na joka kubwa. Lilikuwa likila viumbe wadogo wadogo hadi kunenepa sana, kiasi cha kushindwa kuenea katika shimo lake. Hivyo likalazimika kutafuta shimo jingine. Joka lilifika katika kichuguu cha siafu ..na likasema “Mimi ni nyoka, nina nguvu sana, nipisheni katika shimo hili, nataka kuishi hapa.”  
Pamoja mnaweza!
Siafu wakasema “Tumewekeza nguvu nyingi kujenga mji wetu, tutaondokaje?” Lakini joka likasisitiza waondoke likiwa na uhakika kuwa siafu kwa udogo wao hawawezi kumfanya kitu!
Alikosea. Siafu nao wakatambua udhaifu wao,ila wakapanga mpango, “Tushirikiane wote kwa pamoja” walinong’onezana. Wote wakapanda kwenye mwili wa lile joka, na mara moja wakaenea mwili mzima. Wakaanza kuliuma.
Kuona vile joka likashindwa kuvumilia maumivu na likakimbia kuokoa maisha yake. Kwa umoja, siafu wadogo wakafanikiwa kulishinda joka kubwa.
Kama walivyo Siafu, wakulima walioungana huwa na nguvu na uwezo wa kukabiliana na changamoto ngumu.
Mfano halisi ni wakulima wa miwa wa huko Mtibwa. Mwaka jana walipoona wanalipishwa kodi wasiyostahili, kwa kutumia chama cha wazalishaji miwa cha Mtibwa (MOA) walisimama na kupiga hodi baraza la Kilimo Tanzania (ACT) kutafuta msaada.
“Tuliwaambia ACT kwamba wakulima wa Kilombero wanalipa kodi kidogo kuliko sisi katika iafu wakasema “Tumewekeza nguvu nyingi kujenga mji wetu, utaondokaje?” Lakini joka likasisitiza waondoke likiwa na uhakika kuwa siafu kwa udogo wao hawawezi kumfanya kitu!Alikosea. Siafu nao wakatambua udhaifu wao,ila wakapanga mpango, “Tushirikiane wote kwa pamoja” walinong’onezana. Wote wakapanda
kwenye mwili wa lile joka, na mara moja wakaenea mwili mzima. Wakaanza kuliuma.Kuona vile joka likashindwa kuvumilia aumivu na likakimbia kuokoa maisha yake. Kwa umoja, siafu wadogo wakafanikiwa kulishinda joka kubwa!mzigo wa aina moja wa miwa. Hii haikuwa haki kwetu. ACT walilichukua suala hili na kulifikisha serikalini ambapo Waziri Mkuu aliagiza kodi hizo zirekebishwe, nasi tukapata msamaha,” anasema Hadija Kondo, Mwenyekiti wa MOA.
Unganisheni majeshi,kwa faida ya wote!
Kujiunga katika klab, vyama au makundi kuna manufaa mengi. Na kama hutuamini basi shika haya kutoka kwa Mbunge ambaye ametushirikisha uzoefu wake katika jambo hili.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, anasema pembejeo za kilimo zilichelewa sana
mwaka uliopita hivyo alihakikisha kwamba zinafika mapema msimu unaofuata kwa kuwapa
ushauri wakulima jimboni kwake.
“Niliwaambia waungane na wajipange vizuri. Hakuna njia mbadala katika hili.Mnahitaji kuungana katika kundi kubwa, na kama kungekuwa na shida niliwashauri pia wawahusishe waandishi wa habari kama wanaweza.”
Ushauri wa Zitto unajidhihirisha kuwa na manufaa katika mfano ufuatao. Kikundi cha walikuma cha wanawake kilichojipanga vizuri huko Ijombe mapema mwaka jana walijikuta katika wakati
mgumu baada ya kuambiwa kwamba ardhi waliyokuwa wakilima kwa miaka yote si mali yao
tena.
“Viongozi wa kijiji walikodisha ardhi kwa watu wengine na wakachukua fedha katika mchakato
huu. Tulienda kuomba msaada kwenye Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu kituo cha Mbeya, walikuja na waandishi wa  habari ambao waliripoti juu ya suala hili nakuwapa kashkash viongozi wa kijiji na hatimaye waliturejeshea ardhi yetu,” anasema Salome Simon, Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wakulima cha Ijombe, mkoani Mbeya.
Pengine hili lisingetokea bila nguvu na nia ya dhati ya kina mama wale, na msaada kidogo kutoka kwa Diwani ambaye alihakikisha anakutana na viongozi wa kijiji.
Mfano wa uongozi bora ulionekana! Fedha zilizochukuliwa kutokana na kukodishwa kwa ardhi zilirejeshwa na kupelekwa katika ukarabati wa shule,” anasema Said Mohamed Mwenyeti wa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Mbeya.
Manufaa ya kujiunga na vikundi!    
>Gharama ndogo za uendeshaji: Kama kikundi mnaweza kununua pembejeo kwa pamoja Mara nyingi pembejeo huuzwa kwa punguzo maalum na hivyo mnaweza kuchangia gharama za usafirishaji, hivyo kujiongezea faida! Kuwa Mjanja!
>Nguvu zaidi ya kupanga bei:Kukabiliana na madalali wanopandisha na kushusha bei kiholela.Itakuwa rahisi kama wakulima mtakuwa  wamoja na kuwa na sauti ya pamoja.kama kikundi mnaweza kupanga bei na kulazimisha ikubalike.Tumieni nguvu yenu!    
>Kutenda pamoja (kama siafu):Umoja ni nguvu!kama mna taatizo au mnadhani mmefanyiwa visivyo,msikae kimya,unganisheni nguvu na mzungumze kwa sauti moja.Pamoja mtashinda!  
>Kufanya maamuzi ya pamoja:Kuwa katika kikundi kunawafanya kujifunza na kupata mbinubora za kilimo.Pia mtafanya maamuzi mazuri juu ya masuala yanayowaathiri wakulima wote.Be efficient!   
>Mtaonekana:Serikali za mitaa au kijiji na asasi binafsi zitatambua uwepo wenu kirahisina mara nyingi ni rahisi kusaidia makundi kuliko mtu mmoja mmoja.Kifanyeni chama au kikundi chenu kifahamike.  
>Manufaa mengine ni kwamba unakuwa na kazi chache za kufanya mnapofanya kazi pamoja!
Changamoto hazitakosekana
Wakati mwingine kuna watu hutaka kuwa vinara, msiruhusu hili litokee katika kundi lenu. Msiruhusu mtu mmoja kutumia mwanya huo kwa manufaa binafsi au kuwa na nguvu kuliko wengine. Wekeni mambo wazi kadri inavyowezekana na hakikisheni kila mmoja anawajibika.
Ndiyo, mtu yeyote anaweza kujaribu kukimbia na fedha hivyo ….   
>Kuweni makini na uchaguzi wa wanakikundi, si kila mtu ni mwaminifu!   
>Kuweni na uvumilivu; Kwakweli mnatakiwa kuwa na uvumilivu wa hali ya juu kwa kila mmoja!   
>Ikiwezekana muwe na katiba au muweke sheria zitakazoliongoza kundi lenu ambazo kila mwana kikundi atalazimika kuzifuata!
>Mheshimiane,bila hivyo mambo hayatasonga.
|
Follow us on: