Chezasalama - New Fema
New Fema PDF Print Email

Nilikuwa mama nikiwa na miaka 14-Madam Rita

Nadhani sikuwahi kuwa mtoto,” anasema Rita Paulsen au Madam Rita kama anavyojulikana na wengi. “Yes! Sikuwahi kuwa mtoto maana nilipoanza tu kuufurahia utoto ndipo nilipopokonywa utoto wangu! Kila ninapokumbuka nabubujikwa na machozi,” na ghafla sura yake inabadilika na kuonekana

mwenye huzuni kubwa!

 

 

Si miongoni mwa stori ninazopenda kuzisimulia,lakini kwa faida ya vijana wa Tanzania, hasa wa kike

nitasimulia kwa kuwa sipendi yawakute yaliyonikuta”.Kimya kinatawala tena, anatazama juu darini huku akivuta hisia, kisha anaendelea kusimulia stori yake ya kusisimua .

Ni miaka mingi imepita lakini nakumbuka every single detail! Nilikuwa binti mbichi wa miaka 14, nikiwa Kidato cha Tatu, kwenye shule ya wasichana, huko Uganda. Nilikuwa nafanya vizuri sana darasani kiasi cha kuongoza hata katika kanda nzima.

Mshamba wa ujinsia

Wakati huo sikuwa na ufahamu wowote kuhusu masuala ya ujinsia na ukuaji. Kidogo nilichokuwa nafahamu kuhusu masuala ya wavulana na ujinsia ilikuwa ni story za kusikiasikia kutoka kwa marafiki na dada yangu na ya somo la Biology darasani.

Mama yangu hakuwahi kuniambia chochote maana kimaadili ilikuwa kama mwiko kwa mama kuongelea mambo hayo na mwanae, kwa hiyo mi nilikuwa gizani.

Msukumo rika ndio ulionifanya kukutana na kijana kwenye party ya rafiki, then ‘kilichotokea kikatokea!’ Wakati huo nilikuwa nimeshapata hedhi ya kwanza, lakini kwa kuwa nilikuwa mgeni kwenye issue hizo, sikushtuka nilipokosa kwa miezi iliyofuatia maana nilidhani ni jambo la kawaida kwa binti kukosa hedhi baada ya kuvunja ungo.

Nilikuwa mchezaji mahiri wa netball. Siku moja niliruka sana,nikasikia tumbo limeuma, nilikwenda dispensary lakini kwa udogo niliokuwa nao hata wao hawakudhani ingeweza kuwa mimba, hivyo walisema ni acid na wakanipa dawa. Nilikuwa nasikia kitu kikicheza tumboni lakini sikufikiria kwamba naweza kuwa mjamzito! Maziwa yangu yalianza kujaa lakini dalili zote hizo hazikunishtua! Gossip zilianza kuenea shuleni, nikawa nanyooshewa vidole na hata rafiki zangu wakaanza ‘kucheza mbali’ na mimi!

Siku moja, nilimsikia mwanafunzi mmoja akiniteta kwamba nilikuwa na mimba, nikaenda kumshtaki kwa head girl.Dada mkuu alinisikiliza, kisha akanipeleka chumbani kwake,akaniambia, “Rita, una dalili zote; tumbo na maziwa vimekua,lazima utakuwa na mimba!”

Mamaaaaaaaa! Nilishtuka mshtuko ambao leo hii siwezi kuuigiza! Nilibaki mdomo wazi na katika sekunde chache nilishawaza mengi! Niliwaza nitakavyozaa, nitakavyofukuzwa shule, nitakavyochekwa na kutengwa na familia na jamii yote!Pamoja na yote hayo sikuwahi kufikiria kutoa mimba, niliapa ‘nitakufa’ nayo!

Ilibaki kuwa siri kati yangu na head girl. Wakati huo mimba ilikuwa inakaribia miezi minane. Niliomba ruhusa, nikaenda nyumbani kwa mama Karagwe.

Kasheshe imeanza!

Mama akashangaa kwamba nimekuja ghafla lakini kwa kuwa nilikuwa so innocent, hakuweza kususpect chochote. Nilikuwa nikivaa minguo mikubwa, nikijifunika shuka ili nisigundulike ila mmoja wa anti zangu akagundua. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa balaa! Nilitamani ardhi ifunguke inimeze!

Ilikuwa ni vikao kila siku, mada; Rita na mimba yake. Kila mtu alinishambulia. Mama pekee ndiye aliyekuwa upande wangu ingawa hakuweza kutia neno mbele ya dada na kaka zake! Mjomba alisema “huu ni mkosi katika familia”, akasema nitupwe katika kingo za Mto Kagera, nitajua nitakavyoishi!

Anti yangu mmoja alikuwa akiishi Dar, akapendekeza anichukue ili nikajifungulie kwake nisilete aibu pale kijijini! Mama hakulipenda wazo hilo lakini hakuwa na ubavu wa kulipinga, hivyo lilipita. Stori ya Dar nayo ni mbaya, sitoweza kuisahau.

Sikuweza kuhoji chochote, nilishakuwa traumatized, nilijiona mkosefu so nilikubali kila nilipoambiwa chochote! Stori yangu ni ndefu sana, lakini hatimaye nilijifungua mtoto mzuri wa kike. Baadae nikaondoka kurudi nyumbani kwa mama, Karagwe. 

Mambo yakabadilika!

Mama hakuamini aliponiona, tena nikiwa nimebeba mtoto mzuri,alilia sana. Nilipelekwa kwa baba wa mtoto, alikuwa mdogo kama mimi, hivyo naye aliona ni mazito akatoroka.

Baadaye nikabaki nyumbani nalea mwanangu na wadogo zangu.Mungu si Athumani, dada yangu aliolewa akamchukua mwanangu,ndipo nikaweza kurudi shule.

Safari hii nilikuwa nimeipania shule na sikutaka chochote kiniangushe. Ndoto yangu ilikuwa kuwa lawyer lakini niliona itachukua muda mrefu, hivyo nikaamua kujikita katika masuala ya marketing.

Ajira yangu ya kwanza ilikuwa ITV na ilipotokea nikafukuzwa kazi niliapa kwamba sitoajiriwa tena, bali nitajiajiri mwenyewe.

Nilipokuwa na miaka 23 nikachukua hatua kubwa na kuanzisha kampuni ya Benchmark Production, ambayo ni kampuni binafsi ya kutengeneza video. Baadae nikaanzisha shindano la Bongo Star Search, ambalo limeibua vipaji vingi vya vijana wanaochipukia kwenye muziki nchini.

Ana ushauri mzito kwetu!

Kubeba mimba katika umri mdogo si chaguo sahihi, inaweza kubadilisha ndoto zako kabisa. Lakini, kwa wale ambao yamekwishawakuta, msikate tamaa. Natamani kuona sheria inawaruhusu wasichana waliopata mimba shuleni kuendelea na masomo kwani wanakuwa na ari zaidi ya kuonyesha wanaweza kufanya vizuri. Cha muhimu ni kuwapa vijana wa kike na wa kiume elimu ya ujinsia ili wajilinde na wafanye maamuzi sahihi.

ZAIDI KUHUSU RITA

  • Alizaliwa Karagwe,Murugo,ana damu ya Kisukuma na watu wa Ngara upande wa mama,baba yake ana asili ya Ujerumani.
  • Hajaolewa ila anasema,"sitafuti,lakini akitokea mtu sahihi anataka kunioa siwezi kukataa."
  • Kinachomvutia kwa mwanaume,"I am always attracted to the brain",mengine yote yatajipa tu.
  • Hatasahau siku ambayo mwanae aligraduate digrii yake ya kwanza huko Uingereza,akiwa mwanamke injinia.Anasema alilia machozi ya furaha kwa siku tatu mfululizo.Kwa ujumla Rita ana watoto wawili.
  • Anapenda muziki na shopping!"najipenda,napenda kumpendezesha huyu Rita mnayemwona.

 

 

 

 

 


 

Follow us on:

Your sms voice

JOSEPH M.MWINGIRA - Makambako

Nakipenda kitabu cha Si Mchezo; ushauri wangu ni kuwa elimu mtoayo kuhusu HIV iendane na upimaji

What do you think?

Fadhili - Ruvuma

Je kuhusu kondom hiv zinaweza kuzua VVU.Mbona ziko nyingi za aina tofa

ut,za bei tofaut na zina...
What do you think?

Henry arusha

Femina mko juu sana! AsanteWhat do you think?

Latest news and stuff ....

Umoja ni nguvu
Umoja ni nguvu
Hapo zamani za kale kulikuwa na joka kubwa. Lilikuwa likila viumbe wadogo wadogo hadi kunenepa sana,
Patriotic through design
Patriotic through design
  "I try to work with integrity and be true to my ideas and the people I work with,” says
Si Mchezo 62: Empowering youth through vocational training
Si Mchezo 62: Empowering youth through vocational training
 If you are among those who think vocational training is for young people who have failed to find