Chezasalama - Kuvunja ungo
Kuvunja ungo
Multithumb found errors on this page:

There was a problem loading image /homepages/30/d171144326/htdocs/www/cheza/html/modules/news/fileupload/store/2004-3-4-8-21-47_menstruation.gif
There was a problem loading image /homepages/30/d171144326/htdocs/www/cheza/html/modules/news/fileupload/store/2004-3-4-8-21-47_menstruation.gif

Unakumbuka mshtuko uliopata mara ya kwanza ulipogundua damu katikati ya mapaja yako ? Bila shaka ulikuwa miongoni mwa wasichana wengi ambao walikuwa hawajaambiwa lolote kuhusu hedhi. Hivyo inaelekea ulitishika na ukakosa raha. Na hatimaye ulipopata maelezo ulibaki na hisia kwamba ni mwiko, kitu kichafu na siri iliyofichika. Tulia! Hedhi siyo uchafu wala hatari, hizo ni dalili za asili kwamba msichana anakuwa mwanamke na anaweza kupata ujauzito. Hedhi ni dalili za afya na siyo za ugonjwa.

KUANDAA KIOTA
Kila mwezi mwili unaandaa uwanda wa damu kwenye mfuko wa uzazi, kama kiota laini, iwapo mwanamke atakuwa mjamzito. Kila mwezi ovari inatoa yai linalopita kwenye mfereji na kuingia katika mfuko wa uzazi. Kwa kawaida yai hilo halitakiwi na hufa. Uwanda kwenye mfuko wa uzazi huvunjika na kutoka nje kupitia uke. Hii ndiyo inaitwa hedhi. Kama mwanamke na mwanaume wakijamiiana wakati yai linatolewa,

bila kutumia kinga, manii na yai huenda vikaungana na kutunga mimba. Mimba hiyo itajiweka katika uwanda kwenye mfuko wa uzazi na kuanza kukua. Halafu hedhi husimama, hii ndiyo dalili ya kwanza ya ujauzito.

SIKU ZAKO!
Unapovunja ungo unaweza kuwa na vipindi vya hedhi visivyo na muda maalumu, lakini kadri unavyokua vinajirekebisha. Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28, au mara nyingine kati ya siku 21 na 35. Vipindi vya hedhi vinadumu kwa siku nne lakini vinaweza kuwa vifupi ama virefu zaidi.

MAUMIVU
Unaweza kufanya kitu chochote ulichozoea kufanya wakati wa siku zako za hedhi kama unajisikia vizuri. Lakini baadhi ya wasichana wanapata maumivu makali ya tumbo - fanya mazoezi kwani yanaweza kusaidia kuepuka maumivu ya tumbo. Kama maumivu yanazidi unaweza ukatumia paracetamol au aspirin na kulalia kitu chenye joto tumboni kwako. Baadhi ya wanawake husikia wamechoka, hukasirika au kufadhaika siku chache kabla ya kuanza hedhi. Homoni zinasababisha hisia hizi. Utajisikia vizuri siku zako zinapoanza.

KUJIWEKA SAFI NA TULIVU
Kujiweka katika usafi ni muhimu wakati wa hedhi. Jioshe angalau mara moja kwa siku.Usitumie manukato kwenye sehemu zako za siri kwa kuwa yanaweza kusababisha muwasho. Wasichana wanaweza kutumia vitu mbalimbali kujiweka safi katika siku zao, kama pamba maalumu zilizotengenezwa au vipande vya nguo kuzuia damu. Katika hali ya joto ya Tanzania, inapendekezwa kutumia kinga nje ya mwili kwa ajili ya usafi. Pamba maalum huvaliwa, nje katikati ya miguu lakini ndani ya chupi. Inabidi uzinunue na zinagharimu kati ya sh.600/- na 2,000/-. Ibadili pamba hiyo maalum kila baada ya saa chache ili damu isinuke au kuzaa vi- jidudu. Kama huna fedha ya kununua pamba hizo maalum, unaweza ukatumia pamba ya kawaida ama vipande vya kitambaa. Tengeneza vitambaa vyako mwenyewe vya kinga, kwa kushona vipande vya vitambaa vya pamba ambavyo vinavyonya vizuri. Tumia mataulo ya zamani ya kuogea au vipande vya kanga. Lakini kumbuka yanahitaji kubadilishwa mara kwa mara na kuoshwa kuepusha vijidudu kuingia kwenye uke na kukuletea maradhi !

MILA
Baadhi ya tamaduni zinawaelekeza wanawake kujiweka katika hali fulani tofauti wakati wa hedhi. Wale vyakula maalumu, waache kupika, waache kuswali na wajiepushe na mazoezi yote ya mwili. Wanaelekezwa pia kutokuchanganyika na wanaume. Baadhi ya taratibu hizi ni nzuri kwa sababu zinafanya wanawake wapumzike au kula vyakula vinavyoongeza damu. Lakini nyingine hazina maana na sasa zinabadilika.

BAADHI YA MAMBO KUHUSU HEDHI
Ninaweza kujamiiana wakati wa hedhi? Haishauriwi, hasa inapokuwa bila kinga (kujamiiana bila kondomu). Kama una virusi vya Ukimwi vitakuwa katika damu yako ya hedhi hivyo mpenzi wako anaweza kuambukizwa kirahisi. Lakini na wewe unakuwa hatarini pia. Kama utajamiiana wakati huu na mwanaume mwenye virusi ama magonjwa mengine ya zinaa, unaweza kuambukizwa kuliko wakati mwingine wowote wa mwezi. Kujamiiana kunatibu mkakamao wa hedhi? Hapana, kuingiliana kimwili hakuponyi mkakamao wa hedhi. Hii ni imani tu inayosemwa na vijana. Kama nikifuata kalenda, ninaweza kujua zipi ni siku zangu salama ambapo sitapata mimba? Hapana. Wasichana waliovunja ungo huwa na siku zinazobadilika badilika hivyo hawawezi kutabiri siku zao za salama. Zaidi ya hapo, hakuna siku salama dhidi ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi na magonjwa ya zinaa. Unaweza kuambukizwa magonjwa haya wakati wowote. Usifikirie siku salama kama njia nzuri ya kujilinda!

 

 

Tufuatilie katika

Sauti yako kupitia SMS

JOSEPH M.MWINGIRA - Makambako

Nakipenda kitabu cha Si Mchezo; ushauri wangu ni kuwa elimu mtoayo kuhusu HIV iendane na upimaji

Tuambie maoni yako..

Fadhili - Ruvuma

Je kuhusu kondom hiv zinaweza kuzua VVU.Mbona ziko nyingi za aina tofa

ut,za bei tofaut na zina...
Tuambie maoni yako..

Henry arusha

Femina mko juu sana! AsanteTuambie maoni yako..

Michapo Mipya .....

Umoja ni nguvu
Umoja ni nguvu
Hapo zamani za kale kulikuwa na joka kubwa. Lilikuwa likila viumbe wadogo wadogo hadi kunenepa sana,
Ubunifu wa kizalendo
Ubunifu wa kizalendo
“Najitahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa mwaminifu kwa watu ninaofanya nao kazi,”
Si Mchezo 62: Empowering youth through vocational training
Si Mchezo 62: Empowering youth through vocational training
 If you are among those who think vocational training is for young people who have failed to find