Umebaki muda kiduchu kabla Fema TV Talk Show haijaanza kuruka hewani. Tunafahamu kwamba umesubiri msimu mpya kwa usongo na tunafurahi kukutaarifu kwamba muda mfupi ujao kipindi hichi kitaanza. Kuanzia Februari, yani mwezi wa pili na kuendelea, hakikisha unakaa sambamba na luninga yako:-
Kila Jumamosi saa 1:30 usiku ndani ya ITV: marudio Jumatano saa 7:45 mchana
Kila Jumatatu saa 3:00 usiku ndani ya Star TV: marudio Alhamisi saa 4:30 asubuhi
Vileviele tunafahamu kwamba unahamu kubwa kujua tutatoka na vitu gani. Kama huo ndio ukweli basi bofya maandishi ya rangi ya bluu hapo chini.