|
|
|
|
Wasichana na mabadiliko ya balehe
Mabadiliko haya ni pamoja na:
• Kukua haraka, kiuno kupanuka na matiti kukua • Ngozi kuwa na mafuta mengi, hali inayoweza kumsababishia chunusi • Kuota nywele kwapani na mavuzi • Kuvunja ungo yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza.
Vilevile kuna mabadiliko yasiyo ya kimwili mfano: • Kuongezeka kwa tamaa ya kimwili na mwili kusisimka anapomwona mvulana • Kuanza kutamani wavulana na pia kupenda kujipamba • Kuanza kutoa maamuzi mwenyewe kwani anataka atambuliwe kama mtu mzima anayeweza kuamua bila kusukumwa. Huanza pia kuwa mbishi • Kutokupenda kulazimishwa kufanya shughuli fulani.
Mabadiliko haya ni ya kawaida kwa kila msichana lakini, kila mmoja anabalehe katika muda wake.
| |
 |
 |
 |
Kumbuka, mabadiliko haya humtokea kila msichana na ni yakawaida.
|
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|