|
|
|
|
Kuvunja ungo si ruhusa ya kuanza kujamiiana
Kutoka damu ukeni (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo. Hii ni dalili ya msichana kuingia utu uzima. Msichana akijamiiana kuna hatari ya kupata mimba! Mwanzoni baada ya kuvunja ungo, siku za hedhi zinakuwa na mabadiliko sana. Ni baada ya muda ndipo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi, kwa tarehe ile ile au tofauti kidogo tu.
Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko.Baada ya damu kutoka yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Yai hupevuka ndani ya kokwa kisha husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Mwanamke anapata mimba kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume.Kama yai halikurutubishwa basi hufa na hutangulia kutoka kama ute, na utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu.Hii ndiyo hedhi yenyewe.
Kwa wasichana wengi, mzunguko wao wa hedhi hauna mpangilio katika siku za mwanzoni, hivyo endapo hapati hedhi inayolingana kila mwezi asijali.Katika hali ya kawaida asipopata hedhi na hakujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili.
Hali hii ikiendelea au akiwa na wasiwasi anashauriwa kumwona mtaalamu wa afya.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|