|
|
|
|
Dalili za mtu aliyeathirika
Baada ya virusi vya UKIMWI kuangamiza walinzi wa mwili, yaani chembechembe hai nyeupe za damu, uwezo wa mwili kupambana na magonjwa hupungua.Ina maana kwamba magonjwa mengine yanaweza kuushambulia mwili na mwili kutoweza kujilinda.
Mara nyingi mtu anayeugua UKIMWI anapungua sana uzito, anapatwa na homa za mara kwa mara, anaweza kuharisha mfululizo au anaweza kuwa na vidonda sehemu za siri au mdomoni.Lakini, ukipata dalili moja au mbili kati ya hizi, usiamue mara moja kwamba una VVU.
Yapo magonjwa mengi yanayoonyesha dalili sawasawa na hizi.Unashauriwa kumwona daktari ambaye atakupa ufafanuzi wa kitaalamu.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|