|
|
|
|
Jukumu la kujikinga ni lako
Hakuna chanjo ya kinga ya VVU, lakini kuna aina kadhaa ya tabia inayoweza kusaidia kujikinga na VVU. Kuacha kabisa kujamiiana ni njia mojawapo ya kujikinga na VVU. Kuwa mwaminifu na mpenzi moja asiye na VVU inakusaidia kujikinga. Lakini lazima wote wawili wawe hawajaambukizwa VVU wakati wa kujamiiana kwa mara ya kwanza.
Pia ni vizuri kupata tiba haraka endapo umeambukizwa magonjwa ya ngono, kwani vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya ngono vinarahisisha mwingiliano wa damu au majimaji ya uume au uke wakati wa kujamiiana. Kupitia vidonda hivyo virusi vya UKIMWI vinaweza kuingia mwili ni kwa urahisi.
Kufanya mapenzi salama ni njia nyingine ya kujiepusha na VVU. Mapenzi salama ni yale yanayomaliza hamu bila ya kukutana kimwili au yale yanayohusisha kuchukua tahadhari kwa kutumia kondomu wakati wa kuingiliana kimwili.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|