|
|
|
|
Wadudu kama mbu na maambukizi
Hilo haliwezekani. Mbu na wadudu wengine hawawezi kukuambukiza virusi vya UKIMWI. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye miili yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembe chembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu.
Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na aking ’ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa. Uthibitisho mwingine ni ukweli kwamba sisi sote tungekuwa na virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza virusi vya UKIMWI, kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|