|
|
|
|
Njia mbalimbali za maambukizi ya VVU
Kwa njia yoyote ya kujamiiana iwe ya kawaida au kupitia haja kubwa, katika majimaji ya uke na shahawa kuna kiasi kikubwa cha virusi vya UKIMWI kwa mtu aliyeambukizwa.
Hivyo wakati wa kuingiliana kimwili, virusi vinaweza kuingia kwa mtu asiye na uambukizo kwa kupitia michubuko ya ngozi ya ukeni, sehemu ya haja kubwa au uumeni. Ni rahisi zaidi kupata virusi vya UKIMWI kama wewe au mwenzio ana vidonda ukeni au uumeni
KUONGEZEWA DAMU Mgonjwa mwenye upungufu wa damu akiongezewa damu toka kwa mtu mwenye virusi vya Ukimwi basi mgonjwa huyo nae pia ataambukizwa.
WAKATI WA MIMBA Mama anaweza kumwambukiza mwanae pindi akiwa tumboni, wakati wa kujifungua, wakati wa kukata kitovu na hata kunyonyesha. Uambukizo katika njia hizo nne hutegemea sana kiasi cha virusi katika damu ya mama mtoaji huduma ya uzalishaji na usafi wa vifaa vitumikavyo. Mara nyingi damu huweza kusalia katika vyombo au vifaa hivi baada ya kutumika. Endapo vitatumika bila kutakaswa, ipasavyo vifaa hivi vinaweza kusababisha uambukizo wa magonjwa na hasa VVU.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|