|
|
|
|
Kumwaga shahawa nje, si ngono salama!
Kwa kweli hayo si kweli kwani mwanamume akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa anaweza kuambukiza au kuambukizwa VVU. Kwani mara tu tendo la kujamiiana kuanza kuna majimaji yanayotelewa na mwanaume na pia katika uke wa mwanamke kunakuwa na majimaji.
Kitendo hicho ni hatari kwa mwanamke na pia kwa mwanamume, kwa sababu vijidudu vimo ndani ya majimaji ukeni na uumeni. Hasa kama mmoja kati ya wapenzi ana vidonda au michubuko midogo sehemu za siri, VVU vinaenea kwa urahisi.
KUMBUKA Kutoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa siyo njia salama ya kujikinga na VVU.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|