|
|
|
|
Kuweka akiba
Hisia ambayo mtu anaipata akisikia neno benki ni kwamba majengo makubwa, wanawake na wanaume wakiwa nyuma ya vioo kuangalia kila hatua watu wanavyotembea, lundo la askari kwa ajili ya kuangalia usalama wa watu na fedha zao na hivyo ndivyo alivyokuwa akifikiria kijana Josie mpaka siku alipopeleka mshahara wake wa kwanza benki.
Josie mwenye umri wa miaka 20 kwa woga anaingia kwenye benki, huku akiwa ameshikilia mshahara wake wa kwanza huku akikumbuka maneno ya baba yake, " Tunza fedha na utanufaika." Hofu yake ilikuwa ni zile hisia za mandhari ya benki alizokuwa nazo. Pamoja na woga huo, Josie anakuja benki akiwa makini na pia akijivuna.
Lakini mara alipoingia ndani, maoni yake yalibadilkika. Sura yake ilijawa furaha baada ya kupokelewa na watu wenye sura za kirafiki na tabasamu, ambao walikuwa tayari kumsaidia na kumuongoza. Baada ya wasi wasi wake wa awali, Josie aliweza kufungua akaunti yake ya akiba katika dakika chache tu. Josi alichagua akaunti ile kwa sababu ilikuwa nzuri kwa mahitaji yake. Lakini kuna akaunti aina nyingine pia.
KUNA AINA TATU KUU ZA AKAUNTI Akaunti tatu kuu ambazo ni akiba, ya muda maalumu, na akaunti ya hundi. Akaunti za akiba na za muda maalumu unaweza kuzifungua mwenyewe ama kwa pamoja na mwenzi wako. Akaunti za hundi zinaweza kufunguliwa na watu, makampuni, ubia, klab na vyama. Akaunti za akiba na za hundi zinamwezesha mwenye akaunti hizo kuweka fedha na kuzitoa wakati wowote anapotaka, lakini akaunti ya muda maalum haiwezi kuguswa mpaka muda uliokubaliwa.
Ni fedha kiasi gani unahitaji kufungua akaunti? Kiwango cha chini kinachohitajika kwa ajili ya kufungua akaunti ya akiba kinatofautiana kati ya benki moja hadi nyingine lakini kinaweza kuwa kati ya shilingi 5,000 na 500,000 na kiwango cha riba inayotolewa kwa ajili ya akaunti hii ni kati ya asilimia 4.5 na 8 kwa mwaka.
Akaunti ya hundi inahitaji kiasi cha Shs 100,000 hadi 500,000, kutegemea na benki. Akiba ya muda maalumu inaweza kuwa muda wa mwezi mmoja hadi miaka mwili, na inaweza kutoa riba ya asilimia 4 hadi 10, kwa kutegemea muda ambao fedha zimehifadhiwa kwenye akaunti na taratibu za benki inayohusika. Hata hivyo kiwango cha chini kinachotakiwa na kila benki ni sh. 100,000. Benki siyo tu mahala pa kuweka fedha zako, lakini inaweza kutoa huduma mbalimbali na faida zinazoweza kukusaidia kupanga hali yako ya baadaye kwa uangalifu zaidi. .Unaweza kupata riba kwa fedha zako kwa kuziweka benki na hii inaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mikopo. Mara fedha yako inapowekwa katika akaunti, benki inaweza kufungua hati ya mkopo kwa mwenye akaunti, kuhamisha fedha kwenye akaunti nyingine na kwa wauzaji, au kwa ndugu na marafiki waishio mbali na wewe.
ILI KUNUFAIKA NA HUDUMA HIZI
kwanza fungua akaunti. Hii inaweza kufanyika mara moja kwa kutoa picha mbili za passipoti, kitambulisho ama pasipoti na kuwa na refa mmoja mwenye akaunti kwenye benki husika. .Hati hizi ziwasilishwe pamoja na maombi kutoka benki hiyo. Kama inahitajika akaunti ya biashara, nakala ya hati ya usajili ama leseni inahitajika. Ni mwaka mmoja sasa tangu Josie afungue akaunti yake, na sasa ana kiasi kikubwa cha akiba. Anaamini kwamba kufungua akaunti ulikuwa ni uamuzi wa busara. "Wakati wowote ninapohitaji fedha ninakwenda benki kuchukua. Kwa kiasi fulani najisikia nina nguvu na niko huru". Hata hivyo, Josie ni makini na anatambua kuwa huwezi kuchukua pesa mpaka uwe umeziweka. Hakuna kitu kinachopotea mikononi kwa haraka zaidi siku hizi kama fedha. Nashangaa kwanini wanaiita mshiko maana mshiko hushikika na kuganda mikononi. Lakini siku zote kuna njia katika suala hili kuweka pesa benki. Siyo tu itashikika bali pia itaganda na kuongezeka.
| |
 |
 |
 |
Unafikiri nini kuhusu makala hii? Tupe maoni yako
hapa >> |
 |
 |
» to Top of article
»Back to List
|
|
|
|