|
Chagua swali hapa chini kuona jibu lake!
|
Nikigundulika kuwa nimeambukizwa virusi vya UKIMWI nifanyeje? |
|
Nikipima na kuonekana kuwa sijaambukizwa nifanyaje? |
|
Baada ya kuambukizwa na virusi vya UKIMWI itachukua muda gani mpaka vionekane kwenye damu? |
Nikigundulika kuwa nimeambukizwa virusi vya UKIMWI nifanyeje?
Watu wengine wanaendelea kuishi na virusi hivyo kwa miaka mitano au hata 10. Inategemea mambo mengi kama yalivyotajwa hapo chini. Cha msingi ni kuishi kwa matumaini na kutokata tamaa. Mara nyingi inasaidia kuzungumza na watu wengine wenye virusi vya UKIMWI au na marafiki na ndugu mnaoaminiana sana. Jaribu kuzungumza na mpenzi wako,kwa ajili ya kumpa ujumbe kuhusu kuambukizwa kwako.Yeye vilevile anaweza kuambukizwa na ni vizuri aende kupimwa.
Pia ni muhimu kutimiza misingi ya afya bora kama lishe bora na usafi. Kwa mlolongo huohuo ni lazima utibiwe mara unapopata dalili za ugonjwa wowote. Wenye UKIMWI waache unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kwa sababu unachosha miili yao .Wakijamiiana ni sharti kutumia kondomu, ili kutoambukiza wengine. Akizifuata hatua hizi, mwenye VVU/UKIMWI anaweza kuishi na kuwa na furaha kwa miaka mingi zaidi.
|
Nikipima na kuonekana kuwa sijaambukizwa nifanyaje?
Mara nyingi sana, mtu anayeenda kupima damu kliniki ni tu mwenye wasiwasi kama ameambukizwa virusi vya KIMWI au hapana. wa hiyo, akikipata ujumbe kwamba hajaambukizwa ajiulize kwa nini alikuwa na wasiwasi. Baada ya kufahamu kwamba ni mzima, mtu aliyepima damu aache tabia zile zinazomhatarisha kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Kwa mfano,k ama alijamiiana na wapenzi zaidi ya mmoja bila kutumia kondomu, aache kujamiiana ovyoovyo na atumie kondomu. Ni lazima kuchukua tahadhari zote zinazopasa ili kujiepusha kuambukizwa virusi vya UKIMWI.
|
Baada ya kuambukizwa na virusi vya UKIMWI itachukua muda gani mpaka vionekane kwenye damu?
Baada ya kuambukizwa na virusi vya UKIMWI inachukua muda kama wa miezi mitatu au minne mpaka vionekane kwenye damu kwa kutumia vifaa maalumu ndani ya maabara. Mtu akipimwa damu, amuulize mtaalamu aliyempima damu ni mbinu ipi aliyoitumia na inabidi ajulishwe na miezi mingapi inatumia kwa kutumia mbinu hiyo kutoka kuambukizwa virusi hadi kipimo hicho kutoa majibu sahihi.
|
|