Chagua swali hapa chini kuona jibu lake!
|
Je, kuna uwezekano wowote wa uume kukwama? |
|
Wazee wa umri wa miaka sitini na kuendelea wanajamiiana? |
|
Mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri maarufu kama Chumvi Chumvi, yana madhara gani? |
|
Je, upatapo ashiki, si lazima ufanye ngono? |
|
Nani anastarehe zaidi katika kujamiiana; mwanamke au mwanaume? |
|
Kwa nini mwanamke akigongwagongwa na uume kwenye sehemu ya juu ya uke, hutoa maji maji ukeni? |
Je, kuna uwezekano wowote wa uume kukwama?
Uwezekano huu haupo,kwa sababu uke umetengenezwa na ngozi nyumbufu. Kumbuka kwamba, uke unapanuka kiasi cha kutosha kwa mtoto kupita ukeni wakati wa kuzaa. Hata ukiwa na uume mkubwa hauwezi kukwama ndani ya uke.
|
Wazee wa umri wa miaka sitini na kuendelea wanajamiiana?
Inawezekana kabisa wazee wa umri wa miaka sitini wanajamiiana, ingawa inategemea mtu na mtu. Wengine wanakuwa bado wanayo hamu na nguvu ya kujamiiana na wengine wanakuwa wameishachoka au hawana hamu ya kufanya mapenzi tena. Kila mtu ana utaratibu wake wa kukoma kujamiiana.
|
Mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri maarufu kama Chumvi Chumvi, yana madhara gani?
Kama kati yao wote wawili wanaofanya mapenzi hayo hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara ya kiafya msichana akipokea shahawa mdomoni.Lakini,wasichana wengi hawapendi kupokea shahawa mdomoni na wanasikia kukerwa. Wapenzi wajadiliane kati yao na kuamua kama tendo la kumwaga mbegu mdomoni wanalipenda au hawalipendi. Huu ni msingi mmojawapo wa kujaliana. Hata hivyo,kama mwanaume ameshaambukizwa na magonjwa ya zinaa ni rahisi sana kwa mwanamke kuambukizwa magonjwa hayo.Kwa hiyo, kutumia kondom hata mkitumia mdomo wakati wa kujamiiana ni njia ya kuhakikisha mapenzi yawe salama.
|
Je, upatapo ashiki, si lazima ufanye ngono?
Upatapo hisia za kufanya ngono unaweza kujisahaulisha kwa kufanya mambo mengine kama michezo, kujisomea, kuwasaidia wazazi kazi za nyumbani au kuungana na vijana wenzako katika shughuli za vikundi katika jamii. Vijana wengine huoga maji ya baridi kuondoa ashiki.
Kujamiiana siyo njia pekee ya kukidhi hamu ya kimapenzi. Njia nyingine ni kubusu, kuongea, kushikana mikono, kukumbatiana, kushikana shikana, kupiga punyeto kwa msichana na kwa mvulana.
Punyeto kwa msichana ni kitendo cha kushikashika na kusugua taratibu kinembe chake mpaka anafikia mshindo wakati kwa mvulana ni kusuguasugua uume wake mpaka atoe shahawa (manii). Wengi wapigapo punyeto hufanya hivyo wakiwa peke yao.
PUNYETO INA MADHARA YOYOTE? Kupiga punyeto hakuna madhara yoyote ya kiafya wala kiakili. Kama huwezi kabisa kuacha kujamiiana,hakikisha mapenzi yawe salama. Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa,magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI.
Mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila sehemu za siri za mwanamke na mwanaume kukutana au yale yanayohusisha kuchukua tahadhari wakati wa kuingiliana kimwili.
|
Nani anastarehe zaidi katika kujamiiana; mwanamke au mwanaume?
Siyo rahisi kusema ni nani anayestarehe zaidi ya mwenziwe kwa sababu starehe inayotokana na mwanamke na mwanaume kufanya mapenzi inategemea na watu wote wawili wanaoshiriki katika tendo hili. La msingi katika kujamiiana ni kwa mwanaume kumstarehesha mwanamke kadiri ya uwezo wake na kwa mwanamke kumstarehesha mwanaume kadiri ya uwezo wake. Kama wote wawili wanajitahidi kuburudishana, wote wawili watapata raha sana. Zamani wanaume wengi walifikiri kwamba mwanamke anawajibika kumstarehesha mwanaume na matokeo yake ni kwamba mara nyingi mwanamke hakupata starehe wakati wa kujamiiana. Ili kustarehe, mwanaume na mwanamke wote wanatakiwa kujitahidi kumstarehesha mwenzake.
|
Kwa nini mwanamke akigongwagongwa na uume kwenye sehemu ya juu ya uke, hutoa maji maji ukeni?
Kugusana kwa kutumia viungo vya uzazi ni njia mojawapo ya kuamsha hisia ya kujamiiana. Kama mwanamke anatoa majimaji baada ya kugusana na uume kwenye uke ina maana kwamba ameshikwa na ashiki kubwa. Maji maji hayo yanarahisisha uume kupenya ukeni. Chanzo cha majimaji hayo ni vifuko maalum vilivyomo ndani ya uke.
|