Chagua swali hapa chini kuona jibu lake!
|
Je, mwanamke anayepata hedhi kila mwezi anaweza kuwa tasa? |
|
Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida anaweza kuwa mgumba? |
|
Je, kuna dawa ya kutibu ugumba? |
|
Nifanyeje ili niepukane na ugumba? |
|
Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba? |
|
Je nifanyeje ili niepukane na kuwa mgumba? |
Je, mwanamke anayepata hedhi kila mwezi anaweza kuwa tasa?
Ndiyo, inawezekana kwamba mwanamke anayepata hedhi yake kila mwezi akawa tasa. Pia inawezekana kwamba mwanamke asiyepata hedhi kila mwezi siyomgumba. Ni kweli kwamba kuna uhusiano fulani kati ya hedhi na uwezo wa kupata mimba. Kupata hedhi kila mwezi inamaanisha kuwa mwanamke anao uwezo wa kutengeneza yai kila mwezi.
Hata hivyo siyo rahisi kuwa na uhakika iwapo mirija ya kupitisha yai inaweza kulipitisha yai hilo kutoka kwenye kokwa hadi kwenye tumbo la uzazi. Kwa hiyo hata mwanamke anayepata hedhi kila mwezi anaweza kuwa tasa.
Ili mwanamke awe na uhakika kama ni tasa au la, ni vyema akamwone daktari kwa uchunguzi.
|
Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida anaweza kuwa mgumba?
Ndiyo, mwanaume mwenye uwezo wa kumwaga mbegu bila shida anaweza kuwa mgumba.Kutokuwa mgumba kuna maana kwamba uume wa mwanaume unaweza kusimama, unaweza kumwaga shahawa na kwamba mbegu ni nzima na zina nguvu za kutosha za kurutubisha yai. Kwa hiyo, hata kama mwanaume anamwaga shahawa, inawezekana kwamba hazipo mbegu za kutosha ndani ya shahawa au kwamba mbegu hazina nguvu za kutosha.
KUMBUKA Ni daktari tu anayeweza kumhakikishia mwanaume kuwa yu mgumba au la.
|
Je, kuna dawa ya kutibu ugumba?
Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili kwa sababu tiba inategemea chanzo cha tatizo hilo. Kuna matatizo ambayo yanaweza kutibiwa lakini, mara nyingi ni vigumu au hata haiwezekani kumtibu mwanaume au mwanamke mgumba. Kwanza kabisa, lazima daktari atafute sababu za ugumba kwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa mwanamke na mwanaume wahusika. Baada ya uchunguzi daktari anaweza akawashauri kuhusu uwezekano wa kuwatibu.
|
Nifanyeje ili niepukane na ugumba?
Sababu kuu ya ugumba unayoweza kujisababishia ni kupata magonjwa ya zinaa. Unaweza kuepuka kuwa mgumba kwa kukwepa kuambukizwa magonjwa yazinaa. Unaweza kukwepa maambukizi hayo kwa kutojamiiana au kwa kutumia kondomu kila unapojamiiana. Sababu nyingine za ugumba ni za kimaumbile tangu ulipozaliwa hivyo kuzikwepa haiwezekani.
|
Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?
Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugumba huo kwa mhusika. Kuna matatizo ambayo yanaweza kutibiwa, lakini mara nyingi ni vigumu au hata haiwezekani kumtibu mwanaume au mwanamke mgumba.
Kwanza kabisa, lazima daftari atafute sababu za ugumba kwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa mwanamke na mwanaume. Baada ya uchunguzi daktari anaweza akawashauri kuhusu uwezekano wa kuwatibu. Mara nyingine tiba ni rahisi, lakini matatizo mengine ni matatizo na ni vigumu au haiwezekani kuyatibu.
|
Je nifanyeje ili niepukane na kuwa mgumba?
Sababu kubwa ya ugumba unayoweza kujisababishia ni kupata magonjwa ya zinaa. Unaweza kuepuka kuwa ugumba kwa njia ya kuzuia kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa unaweza kuyazuia kwa njia ya kutojamiiana au kwa njia ya kutumia kondomu kila unapojamiiana. Kuna sababu nyingine za ugumba, nyingine unaweza kuzisababisha na nyingine ni za kimaumbile tangu unapozaliwa.
|