Chagua swali hapa chini kuona jibu lake!
|
Kwa nini damu zinatoka kwenye uke wa msichana? |
|
Kwa nini matiti ya wanawake yanauma wakati yanapokua? |
|
Je, wanawake wanamwaga mbegu kama wanaume? |
|
Nini maana ya kubalehe? |
|
Je, wavulana wanavunja ungo kama wasichana? |
|
Je, nifanyeje ili wengine wasione kwamba nipo kwenye siku zangu? |
|
Mbegu za kiume ni nini? |
|
Je, kuna dawa ya kuwasaidia vijana wa kiume na wa kike waliochelewa kubalehe? |
|
Iwapo kupata hedhi ni dalili kwamba mwili wa msichana unatengeneza mayai, kwanini inaelezwa kuwa msichana huyo hayuko tayari kubeba mimba? |
|
Kwa nini wasichana wengine au wavulana wengine hubalehe mapema na wengine wanachelewa? |
|
Kwa nini matiti yanawake yanauma wakati yanapokua? |
|
Je, tunapobalehe kuna mabadiliko gani ya kimwili kwa msichana? Na pia, tutajisikiaje tukishabalehe kabisa? |
|
Je, uume una urefu gani?`Ni kweli kwamba mwanamme mrefu na mwembamba ana uume mkubwa na yule mnene ana uume mdogo? |
|
Kwanini vijana wanapenda kuzungumzia kujamiiana ? Na kwanini wanapata hamu ya kuwaangalia wenzao wa jinsia tofauti? |
|
Je, unajisikiaje ukifanya mapenzi kabla ya kubalehe? |
|
Sababu zinazofanya wasichana wengi kupata maumivu wakati wa hedhi |
Kwa nini damu zinatoka kwenye uke wa msichana?
Kutoka damu(hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo. Hii ni dalili ya msichana kuingia utu uzima.Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka nane na 18. Lakini kuvunja ungo haina maana kwamba uko tayari kujamiiana. Endapo msichana atajamiiana basi atakuwa kwenye hatari ya kupata mamba.Mwanzo siku za hedhi zinakuwa na mabadiliko sana. Baada ya hapo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo ,wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Idadi ya siku katika mzunguko wa hedhi ni siku 21 hadi 35.Ukitaka kuelewa kabisa maana ya kutoka damu ya mwezi, lazima tueleze kuhusu mzunguko wa hedhi. Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vile vile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi . Mwanamke kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mirija ya kuptishia mayai, inamaana utakuwa umejamiiana siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka. Kama yai halikurutubishwa basi hufa na kutangulia kutoka kama ute na utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu. Hii ndio hedhi yenyewe.Endapo msichana amejamiiana na mvulana na yai likarutubishwa, hataona hedhi na aelewe kamba kuna uwezekano kwamba mimba imetungwa.Wasichana wengi mizunguko yao haina mpangilio mwanzoni, hivyo endapo hapati hedhi inayolingana asijali. Katika hali ya kawaida asipopata hedhi na hakujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili. Hali hii ikiendelea au akiwa na wasiwasi ashauriwe kumuona mtaalamu wa afya.
|
Kwa nini matiti ya wanawake yanauma wakati yanapokua?
Wakati wasichana wanapoingia utu uzima kuna mabadiliko mengi ya kimwili.Wasichana hupata hedhi, huota nywele kwapani, hulainika sauti,hunenepa hasa sehemu za mapajani na pia kukua kwa matiti.Matiti yanapokuwa chembechembe hai zinaongezeka kwenye matiti ili yawe tayari kutengeneza maziwa mara mwanamke anapopata ujauzito.Ongezeko hilo huonekana kama ni uvimbe kwenye matiti. Ni ongezeko hilo la chembechembe mara nyingine husababisha hisia kama maumivu kidogo kwenye matiti, kwa sababu ongezeko la haraka la chembechembe hai linaleta mkandamizo kwenye chembechembe za neva zilizopo kwenye matiti. Huo sio ugonjwa bali hali ya kawaida na hakuna haja ya msichana kuwa na wasiwasi akiona mabadiliko haya. Mara matiti yatakapomaliza kukua, maumivu haya yatatoweka.
|
Je, wanawake wanamwaga mbegu kama wanaume?
Mwanamke hamwagi mbegu kama mwanamme kwasababu kumwaga mbegu ni kitendo cha silka ya binadamu wa kiume tu . Mwili wa mwanamke hautengenezi mbegu wala shahawa . Mwanaume anamwaga mbegu wakati wa kujamiiana na kwasababu ya kutunga mimba. Wakati wa kusikia msisimko au wakati wa kujamiiana katika uke wa mwanamke yanatoka majimaji kidogo, lakini siyo mengi. Majimaji hayo ni dalili ya mwanamke kuwa na msisimko na vilevile yanarahisisha uume kuingia ukeni.
|
Nini maana ya kubalehe?
Kubalehe kunahusisha mabadiliko yanayotokea katika miili ya msichana na mvulana katika kipindi cha ukuaji kuelekea utu uzima. Mabadiliko haya ni ya kimwili, kihisia na kisaikolojia.
|
Je, wavulana wanavunja ungo kama wasichana?
Hapana. Wavulana hawavunji ungo ni wasichana tu. Dalili mojawapo ya wavulana kuingia utu uzima ni kuota ndoto nyevu. Hata hivyo ndoto hizo hazifuati mpangilio au mzunguko maalum.
|
Je, nifanyeje ili wengine wasione kwamba nipo kwenye siku zangu?
Wanawake wengi wanaogopa watu wengine kuona mlembe au pedi anazotumia kujihifadhi akiwa katika siku zake za hedhi. Hata hivyo huna sababu ya kuona haya kuwa uko kwenye siku zako kwani, hayo ni maumbile.
Pamoja na kutokuwa na haja ya kuona haya ni vizuri ukahakikisha kuwa pedi au mlembe unawekwa vizuri katikati ya sehemu zako za siri na chupi ili kuweza kunyonya damu ya hedhi na kutoruhusu kuvuja kuingia kwenye chupi na mwisho kwenye nguo.
Badilisha chochote utakachotumia kama mlembe, pedi,n.k. kila mara kuepusha damu kuvuja na kuacha alama kwenye nguo na kutoa harufu mbaya. Damu ya hedhi inapokutana na hewa hutoa harufu mbaya.
|
Mbegu za kiume ni nini?
Mbegu za kiume zinatengenezwa katika kokwa na ni ndogo sana kiasi kwamba huwezi kuziona kwa macho, lazima utumie darubini. Kila wakati wa kumwaga mbegu, mwanaume anamwaga mamilioni kwa mamilioni ya mbegu katika yale majimaji ambayo yanaitwa shahawa. Shahawa zinatengenezwa katika sehemu maalum mwilini mwa mvulana. Ungeweza kuiona mbegu moja, basi ingekuwa na kichwa kidogo cha duara halafu na mkia mrefu, mwembamba.
Bila mbegu ya kiume mimba haiwezi kutungwa. Kwa ajili ya kutunga mimba, mbegu moja ya kiume inaungana na yai lililopevuka na kulirutubisha.
|
Je, kuna dawa ya kuwasaidia vijana wa kiume na wa kike waliochelewa kubalehe?
Jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba hakuna ubaya wa kubalehe mapema au kuchelewa kubalehe. Hakuna haja ya kuwatibu waliochelewa kubalehe.Watabalehe kama mwingine yeyote yule muda wao utakapowadia. Iwapo utakuwa na wasiwasi na kuchelewa kubalehe unaweza kumwona mtaalamu wa afya au mshauri ili uweze kupatiwa ushauri zaidi.
|
Iwapo kupata hedhi ni dalili kwamba mwili wa msichana unatengeneza mayai, kwanini inaelezwa kuwa msichana huyo hayuko tayari kubeba mimba?
Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini kupata hedhi hakuna maana kwamba msichana yupo tayari kwa kujamiiana au kubeba mimba.Uke wa mwanamke ambaye ni mtu mzima ni madhubuti na unavutika, uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kuvutika sana. Hivyo uke wa msichana unaweza kuchanika au kupasuka wakati wa kujifungua.Vilevile nyonga ya msichana huwa bado nyembamba sana kuweza kupitisha mtoto.
Kwa kuongeza, kupata mtoto siyo suala la mwili kuwa tayari kubeba mimba au kujifungua. Inamaanisha pia kuwa tayari kuwa na mwenzio wa kushirikiana nae katika malezi ya mtoto; kuwa na kipato cha kutosha kutunza familia na kuwa na nyumba ya kuishi. Kwa vyovyote vile kubeba mimba mapema kunamkosesha msichana kuendelea na masomo na hivyo kumnyima nafasi nyingi nzuri za mafanikio.
Hivyo kupata hedhi kila mwezi ni dalili tu za kuelekea utu uzima. Haimaanishi kwamba mwili wake umekuwa vya kutosha kuweza kujifungua mtoto na haimaanishi kuwa amepanga maisha yake kikamilifu kuwa mzazi.
|
Kwa nini wasichana wengine au wavulana wengine hubalehe mapema na wengine wanachelewa?
Kila binadamu duniani ameumbwa tofauti . Wengine warefu na wengine wafupi ,wengine wana rangi ng’avu na wengine wana rangi nyeusi , kwa hiyo, kila binadamu ana namna na muda wake wa kukua .Ni muhimu kukumbuka kwamba hakuna ubaya wowote kubalehe mapema au kuchelewa kubalehe!
|
Kwa nini matiti yanawake yanauma wakati yanapokua?
Wakati wasichana wanapoingia utu uzima kuna mabadiliko mengi ya kimwili.Wasichana hupata hedhi, huota nywele kwapani, hulainika sauti,hunenepa hasa sehemu za mapajani na pia kukua kwa matiti..
Matiti yanapokuwa chembechembe hai zinaongezeka kwenye matiti ili yawe tayari kutengeneza maziwa mara mwanamke anapopata ujauzito.Ongezeko hilo huonekana kama ni uvimbe kwenye matiti. Ni ongezeko hilo la chembechembe mara nyingine husababisha hisia kama maumivu kidogo kwenye matiti, kwa sababu ongezeko la haraka la chembechembe hai linaleta mkandamizo kwenye chembechembe za neva zilizopo kwenye matiti. Huo sio ugonjwa bali hali ya kawaida na hakuna haja ya msichana kuwa na wasiwasi akiona mabadiliko haya. Mara matiti yatakapomaliza kukua, maumivu haya yatatoweka.
|
Je, tunapobalehe kuna mabadiliko gani ya kimwili kwa msichana? Na pia, tutajisikiaje tukishabalehe kabisa?
Wasichana wanaona mabadiliko mengi ya kimwili wakati wa kubalehe kwa mfano: • Kukua haraka, kiuno kupanuka na kukua matiti. • Ngozi kuwa na mafuta mengi, hali ambayo huweza kusababisha chunusi usoni. • Kuota mavuzi kwapani na ukeni. • Kuvunja ungo, yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza.
Na vile vlle kuna mabadiliko yasiyo ya kimwili kwa mfano: • Kuongezeka kwa tama ya kijinsia na hivyo kufanya mwili usisimke anapomwona mvulana. • Katika kipindi hiki huanza kutamani wavulana na pia kujipamba. • Kuanza kutoa maamuzi mwenyewe. Kijana anataka atambuliwe kama mtu mzima. Anaweza kuamua bila kusukumwa na pia huanza kuwa mbishi. Mara nyingi kijana hapendi kulazimishwa kufanya shughuli fulani.
Mabadiliko haya ni ya kawaida kwa kila kijana lakini, usisahau kwamba kila mmoja anabalehe katika muda wake.
|
Je, uume una urefu gani?`Ni kweli kwamba mwanamme mrefu na mwembamba ana uume mkubwa na yule mnene ana uume mdogo?
Wataalamu wanasema kwamba urefu wa uume kwa wastani ni kati ya sentimita saba hadi 10 wakati urefu wa uume uliosimama ni kati ya sentimita 13 had 18. Hata hivyo, si lazima kwamba maumbile ya mtu yawiane na viungo vyake vya uzazi.
Vilevile katika mahusiano ya kimwili jambo la vipimo vya uume si la msingi. Kilicho ni afya nzuri ya watu wote wawili na kupendana kati ya hao wenye mahusiano.Urefu wa uume si muhimu kwasababu sehemu nyingi zinazomridhisha mwanamke haziko ndani ya uke. Kuridhika au kutoridhika wakati wa kujamiiana hakutegemei urefu wa uume.
|
Kwanini vijana wanapenda kuzungumzia kujamiiana ? Na kwanini wanapata hamu ya kuwaangalia wenzao wa jinsia tofauti?
Wavulana na wasichana wanapobalehe mambo mengi hubadilika. Kuna mabadiliko katika maumbile yao; pia katika mawazo na mioyoni mwao. Ni jambo la kawaida kwa anayebalehe kuanza kupata hamu ya wenzie wa jinsi tofauti. Pia ni jambo la kawaida kabisa kuanza kuzungumzia mambo ya mapenzi na kujamiiana.
Kipindi cha kubalehe ndio wakati ambao anaweza kupata habari nyingi kuhusu mambo ya kujamiiana, mambo yanayotendeka mwilini mwake, mawazo yake pia na mawazo ya mwenzie, urafiki wenye msingi wa kuheshimiana na kuaminiana. Hata hivyo hiyo haimaanishi aanze kujamiiana. Kuzungumzia mambo ya mapenzi na kufanya mapenzi ni mambo mawili tofauti.
Kuzungumzia maswala ya mapenzi ni jambo la kawaida kwa wanaobalehe na hakuna madhara kiafya. Kwa upande mwingine, kufanya mapenzi bila kinga kunaweza kusababisha kubeba mimba bila mpango au kupata magonjwa ya kuambukizwa, ukiwemo UKIMWI.
Usije ukaruhusu wenzio wakurubuni ili ujamiiane. Endapo wewe mwenyewe utaona kwamba muda umefika wa kujamiiana hakikisha unachukua tahadhari ya kujizuia kubeba mimba zisizotarajiwa pamoja na kuzuia magojwa ya zinaa.
|
Je, unajisikiaje ukifanya mapenzi kabla ya kubalehe?
Walipoulizwa swali hili vijana wote ambao walijamiiana kabla ya kubalehe wasichana kwa wavulana, walijibu kuwa hawakuhisi chochote na hawakuona uzuri au jambo la ajabu kuhusu kufanya mapenzi. Wengi wao walijamiiana bila kupenda na wengi walisema waliamua kufanya hivyo kwasababu wenzao walifanya na hivyo kupata msukumo na kujaribu. Kwa kusubiri na kutofanya mapenzi hadi umekuwa mtu mzima hupati hasara yoyote.
Wakati mwingine inakuwa vigumu sana kukataa kufanya mapenzi kutokana na msukumo kutoka kwa wenzio. Hata kama unajiona uko tayari, mara nyingine inakuwa siyo rahisi kusema hivyo. Endapo utafanikiwa kushinda ushawishi, unastahili kupongezwa na ni jambo la kujivunia kwa sababu unaweza kufuata utashi wako.
|
Sababu zinazofanya wasichana wengi kupata maumivu wakati wa hedhi
Wakati wa kupata hedhi msichana huwa na mabadiliko katika via vyake vya uzazi.ambao ulikuwa tayari kupokea mimba na kuvunjika kwa yai ambalo halikurutubishwa. Damu ndani ya mfuko wa uzazi hufanya misuli ya mfuko huo kuanza kujikamua ili damu itoke nje, kujikamua huko kwa kizazi ndiyo hasa ya maumivu hayo.
Iwapo maumivu yatakuwa makali sana na pengine kutoka kwa damu nyingi kuliko kawaida au kuendelea na na hedhi kwa siku zaidi ya sita, basi hii ni dalili ya kuwa na tatizo. Inashauriwa msichana amwone mtaalamu wa afya kwa uchunguzi zaidi.
|